Kijiji India Chasherehekea Ushindi wa Kamala Marekani
WAKAZI wa kijiji cha Thulasendrapuram kusini mwa India, wamesherekea ushindi wa Makamu wa Rais Mteule wa Marekani, Kamala Harris, ambaye ana asili ya India. Mama wa Kamala anatoka kwenye kijiji hicho.
Wanakijiji hao wamekuwa wakitandika khanga na kuweka mabango na picha za Kamala kwenye barabara na kufanya ibada kabla ya uchaguzi ili yeye na mgombea urais Joe Biden washinde.
Kamala atakuwa mwanamke wa kwanza mwenye asili ya Mmarekani mweusi na Mhindi kushika wadhifa huo mkubwa. Mama yake Kamala ni Mhindi kutoka India na baba ni Mmarekani mweusi kutokea nchini Jamaica.
Haris anakuwa mtu wa kwanza Mu-Asia kuwa Makamu wa Rais wa Marekani. Mama yake alizaliwa India lakini baadaye akahamia Marekani kwenda kusoma akiwa na miaka 19 .