The House of Favourite Newspapers

Kilichotokea Leo Mahakamani Polisi Waliosindikiza Dhahabu Mwanza

SHAURI namba 1/2019 la uhujumu uchumi, rushwa na kutakatisha fedha dhidi ya watu 12 wakiwemo askari polisi wanane katika mahakama ya hakimu mkazi Mwanza limetajwa leo Jumatatu Januari 28, 2019 na kuahirishwa hadi Februari 11, 2019 kwa kuwa upelelezi haujakamilika.

 

Wakili wa Serikali, Castus Ndamugoba,  ameiambia Mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Kwa mara ya kwanza, washtakiwa walifikishwa mahakamani Januari 11, 2019 wakidaiwa kuhusika na sakata la kilo 319.59 za dhahabu yenye thamani ya zaidi ya Sh.  bilioni 27.018 na fedha taslim Sh. milioni 305 zilizokamatwa zikisafirishwa kutoka Mwanza kwenda Geita.

Mbele ya hakimu mkazi, Gwai Sumaye, mawakili watatu wa serikali, Castus Ndamugoba, Robert Kidachi na Jackline Nyantoro,  waliieleza mahakama kuwa washtakiwa walitenda makosa hayo kati ya Januari 4 na 5, 2019.

Wanaokabiliwa na shauri hilo ambao hawakutakiwa kujibu lolote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo kisheria wa kusikiliza shauri hilo, ni aliyekuwa mkuu wa operesheni mkoani Mwanza, mrakibu mwandamizi wa polisi, Morice Okinda, E. 6948 D/CPL. Kasala, F. 1331 PL. Matete, G. 6885 D/C Alex na G. 5080 D/C Maingu.

Wengine ni G. 7244 D/C Timothy, G. 1876 D/C Japhet, H. 4060 D/C David Kadama, Hassan Saddiq, Emmanuel Mtemi, Kisabo Nkinda ambaye pia anafahamika kwa jina la Paulo Nkinda na Sajid Hassan.

Comments are closed.