Kim Kardashian Amekiri kuulaghai Umma

MWANAMITINDO na Staa wa Reality show Kim Kardashian amekiri kuulaghai umma kipindi ambacho alikuwa akitafuta upenyo wakutoboa kwenye tasnia ya Entertainment.

Kim alikiri hayo kwenye show ya Tv E Entertainment ambayo hurusha Show ya E Hollywood story kupitia mtandao wa YouTube na kusema kuwa aliwahi kudanganya kuwa amekula chakula cha usiku na Britney Spears.
“Nilikuwa hotelini na rafiki yangu na nikagundua kuna mapaparazi nje ya mlango wetu na hiyo ilitokana nauwepo wa star Britney chumba cha jirani na chakwetu”, alisema kardashian

Huku akicheka kim aliongeza kuwa ilibidi watoke nje na kushauriana na rafiki yake kuwateka mapaparazi hao kuwa yeye ataenda kuonana na Britney
“Nilitoka nje huku naongea na simu, nikidai kuwa tutaonana mgahawani baadae kidogo, na nililitaja jina la Britney mara kadhaa ilikupata attention yao, na kweli nilifanikiwa kwani Asuvuhi yake nilikuwa gumzo kuwa Nilipata Dinner na Britney Spears”.

Kim aliiambia E kuwa akiwa mzee atafurahia sana kutengeneza Reality Show yake yeye binafsi, kwani yapo mengi ambayo watu hawafahamu kumuhusu.


Loading...

Toa comment