The House of Favourite Newspapers

Kimenuka Mbeya: Agizo la Mkuu wa Mkoa, Machinga Wagomea!

Hali si shwari katika Jiji la Mbeya, maeneo ya Mwanjelwa, kufuatia Mkuu wa Mkoa huo, Albert Chalamila kuwataka wamachinga kuyahama maeneo wanayofanyia biashara  na kuelekea maeneo rasmi yaliyotengwa na Serikali (Soko Kuu la Mwanjelwa na Stand ya Nane Nane).

 

Mapema leo Jeshi la Polisi lililazimika kuingilia kati na kutuliza ghasia za wafanyabiashara hao ambapo wamepinga agizo hilo la Mkuu wa Mkoa wakidai hapo ni eneo ambalo wamelizoea miaka yote.

 

Aidha, RC Chalamila amewataka wawe wamehamisha biashara zao hadi kufika Ijumaa saa 10 na kwenda maeneo rasmi.

 

Mpaka sasa soko Kuu la Mwanjelwa limefungwa kufuatia ghasia hizo ambapo machinga hao walifunga barabara inayoelekea Hospitali ya Mwanjelwa lakini hakuna majeruhi wala madhara yaliyoripotiwa kutokana na tukio hilo mapaka sasa, tutaendelea kuwapa taarifa kadri tutakavyozipata, endelea kuwa nasi.

INAUMA! Mama Asimulia Alivyobakwa, Akatobolewa Macho!

Comments are closed.