The House of Favourite Newspapers

KIMENUKA! NDOA YA PILI YA SIRI YA Z-ANTO MAJANGA YAMKUTA

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Ally Mohamed Ahmad ‘Z-Anto’ hivi karibuni alikwaa skendo baa­da ya kudaiwa kuoa mke mwingine (wa pili) kwa siri huku mke mkubwa aliyejulikana kwa jina la Sara ak­ichachamaa, hata hivyo ndoa hiyo imeibua mapya.

 

Habari zinadai kuwa mwana­muziki huyo hivi karibuni alifunga ndoa na dada wa msanii wa filamu, Wastara Juma aitwaye Naima huku mke mkubwa akiwa hajui, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa Dini ya Kiislamu.

 

“Niwaambie tu kwamba hivi ka­ribuni Z-Anto alifunga ndoa ya siri bila kumwambia mkewe ambapo amemuoa dada yake Wastara anayejulikana kwa jina la Naima, mke mkubwa akazifuma picha ndiyo siri ikafichuka.

 

“Umetokea ugomvi mkubwa kati ya Z-Anto na mkewe huyo kwa sababu hakumwambia kwamba anaoa mke wa pili hivyo mwanamama huyo anaumia sana na anamlaumu Wastara kwamba yeye ndiye aliyemku­wadia mumewe kwa dada yake hivyo anafanya utaratibu aende Bakwata kumshtaki mumewe,” alidai mtoa habari aliyehudhuria ndoa hiyo.

 

MKE ACHACHAMAA!

Akizungumza na Ijumaa Wik­ienda, mke wa Z-Anto alisema alikuwa anakuta meseji kwenye simu ambazo mumewe huyo alikuwa akiwasiliana na huyo Naima akawa anamuuliza lakini anakuwa mkali, baadaye aligun­dua kuwa walishafunga ndoa.

Baada ya hapo maelewano ny­umbani yakawa ‘ziro’ hivyo yeye akiwa ni mwanamke anayejita­mbua wala haoni shida, utafuata taratibu za ndoa kisha kuyaacha maisha yake yaendelee.

 

Z-ANTO ANASEMAJE?

Baada ya gazeti hili kupata habari hizo na mkewe kutoa yake ya moyoni, wanahabari wetu walimtafuta Z-Anto ambapo ali­funguka kuwa habari hizo hazina ukweli.

“Niwaambie tu kwamba hizo habari za mimi kuoa hazina ukweli, mimi na mke wangu tuko vizuri kabisa hatuna tatizo ila kama anasema ameenda Bak­wata mimi ndio kwanza nawasi­kia nyie.

 

“Ningekuwa nimeoa ningeweka wazi tu lakini hakuna kitu kama hicho, kuhusu kuwa karibu na familia ya Wastara ni kwamba nil­ianza urafiki na familia hii kama miaka 10 iliyopita, nilikuwa nam­fanyia dua mume wa Wastara marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ alipokuwa anaumwa,” alisema Z-Anto.

Kuhusu picha zake na Naima za ndoa zilizosambaa kwenye mitandao, msanii huyo alisema kuna kitu walichokuwa wana­kifanya kuhusiana na sanaa ambacho kwa sasa hawezi kukiweka wazi.

 

MSIKIE NAIMA

Dada wa Wastara, Naima al­ipoulizwa kuhusiana na hilo na picha za ndoa yake na Z-Anto zilizosambaa mitandaoni alikuwa na haya ya kusema;

“Jamani mimi nina mume wangu, sijafunga ndoa na Z-Anto, zile picha nilienda kupiga yeye akiwa ni msimamizi tu wa harusi nyingine ya mtu lakini siyo ndoa yangu, ingekuwa ndoa ninges­ema maana ni jambo la heri huwezi kuficha.”

 

NENO LA MHARIRI

Kila mmoja amekataa kufungwa kwa ndoa hiyo, Ijumaa Wikienda bado linausaka ukweli na iwapo litaubaini kwa mapana zaidi litarudi tena kueleza kwa undani.

Comments are closed.