The House of Favourite Newspapers

Kimenuka: Viongozi Wawili Chadema Wavuliwa Uanachama

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimewavua uanachama viongozi wake wawili ambao ni aliyekua Naibu Katibu Mkuu Bara, Getrude Ndibalema na Mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Kilimanjaro, Dickson Kibona, baada ya kubainika kuwa wanakisaliti chama hicho.
 
 
 
Akizungumza jana Mei 21, na wanahabari jijini Arusha, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema, Patrick Ole Sosopi, alisema uamuzi huo umekuja baada ya kufuata taratibu zote za kuwahoji kupitia tume iliyoundwa na kuwahoji baada ya kuwepo tuhuma za usaliti ambalo ni kosa kubwa kwenye chama hicho.
 
 
Sosopi amesema Bavicha imeridhia kuwaondoa wanachama hao baada ya kujiridhisha kwa makosa waliyoyafanya.

Comments are closed.