The House of Favourite Newspapers

Kimenuka… Wabunge wa Tanzania, Burundi Wamkataa Spika wa EALA

SIKU moja baada ya Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika mashariki kuchaguliwa na wajumbe wa nchi nne za jumuiya badala ya sita wabunge kutoka Burundi na Tanzania na Burundi wamesema uchaguzi huo umekiuka misingi na kanuni za Jumuiya hiyo.

Wakizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha, Mwakilishi wa wabunge hao wamesema hakukuwa na sababu ya kutumia nguvu jazba na uharaka wa kumchagua Spika kabla ya hoja zao ikiwemo ya kutaka kupata ufafanuzi wa mzunguko wa kumpata spika haujatolewa na kwamba hawakubaliani na na suala hilo na endapo  hali isipodhibitiwa malengo ya kuundwa kwa jumuiya hiyo hayatatimia.

 

Kwa upande wao Wabunge kutoka Tanzania wamesema hatua ya wabunge wa bunge hilo kuanza kukiuka viapo vyao muda mfupi baada ya kuapishwa ni dalili za kukosa moyo wa uvumilivu, umoja, na ushirikiano wa dhati ambao kwa muda wote ndio umekuwa msingi wa jumuiya hiyo na sio dalili nzuri hasa ikizingatiwa kuwa miongoni mwa malengo ya jumuya ni kudumisha mshikamano na kwamba kilichofanyika ni sio kumchagua Spika bali ni maoni yao kuwa Mh. Martin anafaa kuongoza.

 

Aidha Wabunge wa Tanzania wamesema kuwa wanaendelea kuziomba ngazi zinazohusika kuangalia upya suala hilo na kutoa nafasi ya majadiliano kwani ndio msingi wa kupata suluhu.

Kufuatia hali hiyo wabunge kutoka Burundi licha ya kudai kuwa hawamtambui Spika aliyechaguliwa wamesema hawawezi kushiriki kikao chochote kitakachoendeshwa na spika huyo.

 

Wabunge hao wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliapishwa siku ya tarehe 18 /12 /2017 na wakati wa kumchagua spika uliibuka mjadala unaodaiwa kusababishwa na taarifa zilizotolewa na katibu wa Bunge kuwa wabunge wa nchi zote ispokuwa uganda wanaweza kuomba kugombea uspika wakati utaratibu wa awali ulikuwa ni wa kufuata mzunguko.

Wabunge hao wamefafanua kuwa hata kama mzunguko ungezingatiwa bado lingehitaji ufafanuzi ambao ungezihusisha Burundi, Rwanda na Sudani Kusini suala ambalo wanasema licha ya kuliwasilisha lilipuuzwa.

Comments are closed.