The House of Favourite Newspapers

KING Monada Alivyoiteka Afrika na ‘Malwedhe Idibala’ Staili ya Kuanguka

IWE ni mitandao ya kijamii yaani WhatsApp, Instagram, Twitter kote ukikutana na vipande vya video ya muziki ni wazi itakuwa watu wanacheza wimbo huku wanaanguka na kusimama muda huohuo. Ulishajiuliza wimbo huu kaimba nani na staili hiyo inaitwaje?

 

Aliyewateka anaitwa Khutso Steven Kgale a.k.a King Monada na wimbo unaitwa Malwedhe na kama ulikuwa hujui ile staili ya kuanguka na kusimama haraka inaitwa Idibala ikiwa na maana ya kuanguka (collapse).

King Monada ukimuona huwezi kudhania kama ndiye mkali wa wimbo huo, anatokea kwenye kijiji cha kimaskini kilichopo Mokgolobotho huko Limpopo nchini Afrika Kusini.

 

Kutokana na kukulia familia ya kimasikini, wazazi wake hawakuwahi kubahatika kusoma na ndiyo maana hata haijulikani King Monada alizaliwa mwezi upi na mwaka gani.

Kingine ambacho hujui, akiwa mtoto alipenda sana kuimba na kucheza na mwaka 2004 alianza kupenya mdogomdogo na baadaye akaachia Ngoma ya Ska Bhora Moreki iliyoteka kisawasawa na kumpatia tuzo tatu kwa mpigo za FAME SA 2016 sambamba na kuwa wimbo bora wa mwaka ambao ulimuingizia kiasi cha randi milioni 10 (zaidi ya bilioni 1.5 za Kibongo) ndani ya mwaka mmoja.

 

Huyo ndiyo King Monada aliyeiteka Afrika kuanzia Nigeria, Zimbabwe, Botswana, Kenya na sasa Bongo na staili ya Idibala huku tahadhari zikitolewa kwa wale wanaoendesha magari wakicheza staili hiyo.

King Monada Malwedhe [New Hit 2018]

Comments are closed.