The House of Favourite Newspapers

KISA MKWANJA WA MUMEWE MPYA, NAWAL AAMUA KUFUTA TATTOO YA NUH!

0
Nawal na mumewe mpya.

Baada ya Jini Mkatakamba kuipitia ndoa ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda, aliyekuwa mkewe Nawal amefunguka kuwa yupo katika harakati za kuifuta tattoo ya Nuh aliyoichora mkononi mwake.

Nawal ambaye baada ya kuachana na mzazi mwenziye Nuh Mziwanda, ameolewa tena na mwanaume anayefahamika kwa jina la Masoud, amefunguka Kwa kusema; “Nitaifuta tattoo ya Nuh Mziwanda, mume wangu ana fedha, atanipa ili niende kuifuta.”

Nawal na Nuh Mziwanda.

TUJIKUMBUSHE KIDOGO

Baada ya kutemana na Shilole, Nuh Mziwanda aliingia katika uhusiano wa kimapenzi na Nawal  ambapo Novemba, 2016,  walifanikiwa kufunga ndoa na wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike anayeitwa Anyaghire.

Hivi karibuni ndoa yao ilivunjika baada ya kupitiwa na jini mkatakamba, kwa kile kinachodaiwa kuwa Nuh amerudi katika dini yake ya Kikristo na kwa kufanya hivyo ni kama amemkana mkewe aliyemuoa kwa dini ya Kiislamu, ambapo baada ya kutengana kwao, Nawal akaolewa tena na mwanaume anayefahamika kwa jina moja la Masoud.

NA ISRI MOHAMED/GPL

 

Wapiga Debe Wafunguka Baada ya Serikali Kuwatoa Kwenye Vituo

Leave A Reply