The House of Favourite Newspapers

KISUTU: Kaburu Achukuliwa na TAKUKURU

TASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imemchukua Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ kwa ajili ya kumuhoji kuhusiana na tuhuma zinazomkabili za utakatishaji fedha kiasi cha Dola za Marekani 300,000 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

 

Katika Kesi hiyo, mshtakiwa mwingine ni Rais wa Klabu hiyo, Evans Aveva ambaye yeye hakuweza kufika mahakamani hapo kutokana na kwamba leo haikuwa tarehe maalum ya kesi hiyo.

 

Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kwamba kesi hiyo haikupangwa leo isipokuwa wamemtoa Kaburu gerezani kwa kibali ili akahojiwe.

 

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa alimkabidhi Kaburu kwa Wakili Swai huku akimtaka amrudishe leo hii hii kama alivyoomba, ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 25, mwaka huu.

 

Aveva na makamu wake, Geofrey wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha USD 300,000. Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa walikula njama ya kughushi fomu ya maombi ya kuhamisha fedha ya Machi 15, 2016 wakionesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa USD 300,000 kwa Evans Aveva wakati si kweli.

NA DENIS MTIMA | Global Publishers

SIMANZI! Esha Buheti, Batuli Wamlilia Mama Johari

Comments are closed.