The House of Favourite Newspapers

Kiungo wa Manchester United Matic Atangaza Rasmi Kuondoka Klabuni

0
Kiungo wa Manchester United Nemanja Matic ametangza kutimka klabuni hapo mwisho wa msimu huu

KIUNGO mkabaji wa klabu ya Manchester United raia wa Serbia Nemanja Matic amesema mwisho wa msimu huu anaondoka katika klabu hiyo.

 

Matic ameandika kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram na kusisitiza kuwa ilikuwa ni heshima kubwa sana kake kuichezea klabu hiyo.

 

“Baada ya kufikiria sana, nimeamua kwamba msimu huu utakuwa wa mwisho kangu na Manchester United, imekuwa ni heshima kubwa kuichezea klabu hii na ntafanya kila kitu kuwasaidia wachezaji wenzangu tumalize msimu huu vizuri kadri iwezekanavyo.”

 

Nemanja Matic alisajiliwa na Manchester United akitokea klabu ya Chelsea ambako alifanikiwa kupata makombe mawili ya Ligi Kuu nchini Uingereza, Kombe la FA pamoja na Capital one.

Nemanja Matic Kiungo wa Manchester United na timu ya taifa ya Serbia

Kwa sasa Manchester United ipo nafasi ya 7 katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza huku jumamosi hii ikiwaalika Norwich katika uwanja wao wa Old Trafford mchezo utakaopigwa saa 11 jioni kwa saa za Afrika Mashariki

 

Leave A Reply