The House of Favourite Newspapers

Kocha wa Liverpool Awaonya Real Madrid -Video

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ameitahadharisha klabu ya Real Madrid kuelekea mchezo wao wa fainali wa klabu bingwa barani Ulaya hapo leo Mei 26, 2018.

 

Klopp amesema kuwa anafahamu fika klabu yake haina uwezo mkubwa kulinganisha na wapinzani wao Real Madrid lakini hiyo siyo sababu kwa Madrid kuwapeza kwani wana historia nzuri kwenye mechi kubwa.

Sisi ni Liverpool sisi ni Liverpool tunafanya vizuri kwenye mechi kubwa. Hakuna aliyejua kama tutafika hapa lakini leo hii tupo hapa na hii ni kwa sababu sisi ni Liverpool.“amesema Jugen Klopp kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari jioni ya jana mjini Kiev, Ukraine.

 

Wengine waliotoa mitazamo yao ni wachezaji wa Liverpool, Van Dijk na Nahodha Jordan Brian Henderson ambao wote wamekiri kuwa gemu ni nzito ila wataushangaza ulimwengu.

Tazama press hiyo hapa chini na kuangalia wachezaji wa liverpool wakifanya mazoezi yao ya mwisho kuelekea kesho kwenye fainali vs Real Madrid.

Comments are closed.