KOLETHA, BEN BRANKO NUSURA WAZICHAPE

NI shida! Mkongwe wa filamu za Kibongo, Koletha Raymond na msanii mwenzake, Ben Branko hivi karibuni waliponea chupuchupu kuzichapa baada ya kupishana kwa maneno. Chanzo kilichokuwa eneo la tukio kilieleza kuwa, Koletha na Ben nusura kuzichapa ndani ya Ukumbi wa TZF uliopo Kigogo, Dar wikiendi iliyopita walipokuwa katika kikao.

“Ben alianza kumtukana matusi ya nguoni Koletha ambapo walitaka kupigana ila kilichosaidia ni Koletha kuwa mpole na watu waliokuwepo wakatuliza, lakini kama siyo hivyo tungekuwa tunazungumza mengine sasa hivi,” kilisema chanzo.

Ili kuujua ukweli kuhusu hilo, Amani liliwatafuta wahusika ambapo aliyepatikana ni Koletha ambaye alitoa ufafanuzi na kusema ni kweli kulitokea kutokuelewana ndipo Ben akaanza kumtukana matusi ya nguoni, jambo ambalo lilimkera vilivyo kwani hakumkosea chochote.  “Namshukuru Mungu, nilikuwa mpole maana ilikuwa kidogo tu tupigane, nikamwepusha shetani kwa kukaa kimya, yeye Ben akawa ananitukana tu, sijui alikuwa ana hasira za nini,”alisema Koletha. Kwa upande wa Ben alipotafutwa kwa njia simu iliita tu bila kupokelewa


Loading...

Toa comment