The House of Favourite Newspapers

Korea Kaskazini Yazindua Kombora Jipya

0

TAIFA la Korea Kaskazini limezindua kombora jipya la masafa marefu linaloweza kurushwa kutoka kwenye manowari ambalo vyombo vya habari vya vya taifa hilo vimelielezea kuwa kama ‘kombora lenye uwezo mkubwa duniani’.

 

Picha zilizotolewa na vyombo vya habari vya Korea Kaskazini zilionyesha makombora manne makubwa yenye rangi nyeusi na nyeupe yakiendeshwa na kupitishwa mbele ya rais huyo huku kundi kubwa la watu likipunga mikono.

 

Makombora kadhaa ya aina hiyo yalionyeshwa katika gwaride la kijeshi ambalo limeshuhudiwa na kiongozi wa taifa hilo, Kim Jong Un, viliripoti vyombo vya habari vya taifa hilo.

Hatua hiyo imekuja kufuatia mkutano wa kisiasa usio wa kawaida ambapo  Kim aliitaja Marekani kama ‘adui yake mkubwa zaidi’.

 

Onyesho hilo la kijeshi linajiri siku chache kabla ya kuapishwa kwa rais mteule wa Marekani,  Joe Biden.

 

Leave A Reply