The House of Favourite Newspapers

Kotei Aomba Radhi Tukio la Kumpiga Konde Gadiel Michael – Video

MCHEZAJI wa Simba, James Agyekum Kotei (25), Raia wa Ghana, amewaomba radhi mashabiki, wapenzi na wadau wa soka kutokana na kosa alilolifanya kwenye mchezo wa timu yake dhidi ya watani wao wa jadi Jumapili iliyopita baada ya kumpiga ngumi mchezaji wa Yanga SC, Gadiel Michael.

Katika tukio hilo ambalo limeibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii huku wadau wengi wa soka wakisema Kotei hakufanya kitendo cha kiungwana na si cha kimichezo baada ya kumshushia ngumi ya shingo Gadiel walipogongana wakigombania mpira.

Hayo yamejiri ikiwa ni takribani siku moja tangu klabu ya Yanga itoe tamko kwamba ingependa kumsikia Kotei akiomba msamaha hata kama ni kupitia mitandao ya kijamii huku klabu hiyo ikibainisha kuwa tayari imeshapeleka malalamiko yao kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili waone cha kufanya.

Simba nao hajakaa kimya, kupitia ukurasa wao wa Twitter wameomba radhi na kuandika;

“Tunapenda kumwombea radhi mchezaji wetu James Kotei kwa mchezaji Gadiel Michael pamoja na Watanzania wote kwa kitendo alichomfanyia katika mchezo wa Ligi Kuu baina ya Simba na Yanga uliopigwa siku ya Jumapili katika Uwanja wa Taifa.”

Shuhudia Kotei alivyompiga Gadiel.

View this post on Instagram

 

Huu ni uungwana wa mchezo?

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

THOMAS ULIMWENGU AFUNGUKA MAISHA YAKE YA SOKA SUDAN

Comments are closed.