The House of Favourite Newspapers

KUBWA KULIKO: MAKONDA Agawa Kiwanja Kwa YANGA – Video

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenye tamasha maalumu la kuichangia klabu ya Yanga ambalo limefanyika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam amesema:-

“Mimi sijaja hapa kama mshabiki wa mpira bali kama serikali nimeona utatatibu haukufuatwa mmefanya jambo kwenye Mkoa wangu bila kunishirikisha lakini nimeona nia ya dhati ya Yanga kufufuka upya.

 

“Ninaelewa umuhimu wa timu kubwa kama hizi zinapofanya michezo katika Mkoa wetu kwasababu uchumi unajengwa na michezo pia hivyo nimetafakari kama serikali ninawapa Yanga uwanja Kigamboni.

 

“Kuanzia Jumatatu nitakuwepo ofisini na wataalamu wa ardhi ili mtupatie nyaraka zenu tuwape eneo mjenge uwanja wakati Simba wanaenda Mwabwepande Yanga wanaenda Kigamboni tunakutana uwanja wa Mkapa ,” amesema Makonda.

Comments are closed.