The House of Favourite Newspapers

Kumekucha: Zari Amvua Nguo Tanasha

DAR ES SALAAM: Kumekucha tena! Ni maneno ambayo yanaweza kutumika kuelezea dude lililoamshwa linalomhusisha, zilipendwa wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abbdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na mpenzi wa sasa wa mwanamuziki huyo, Tanasha Donna, twende taratibu na Risasi Jumamosi, utaelewa tu!

 

Iko hivi, kama si mtundu sana wa mitandao ya kijamii, si rahisi sana kupata ubuyu kwa wakati sababu kuna mambo yanatokea na usipokuwa ‘online’ wakati huo, huwezi kupata ‘connection’ itakayokuunganisha na tukio lililotokea wakati wewe haupo online.

 

MAMBO YALIVYOIBUKA

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, juzi Zari alitupia picha ambayo ilimuonesha mkononi ameshika simu aina ya  Samsung na ndipo mjadala ulipoanzia hapo. Kwenye komenti mbalimbali za watu, aliibuka shabiki mmoja anayejiita Theddyofficially ambaye alimchokoza Zari kwa kumgusia jambo kuhusu Tanasha. “Nilichogundua kwa mama Tee hanaga shobo za kupaparikia simu mpya za iPhone 11 Pro kama wakina naniii, yeye simu yake ileile pendwa,” alichochea moto shabiki huyo.

UFAFANUZI KIDOGO…

Japo hakumtaja jina lakini wataalam wa mambo huko Instagram waliweza kung’amua kwamba, Theddyofficially alikuwa anamtupia dongo Tanasha ambaye juzikati amezawadiwa simu ya iPhone 11 Pro na Mondi baada ya kujifungua.

MAJIBU YA ZARI SASA…

Baada ya shabiki huyo kumchokoza Zari, kwenye uwanja huohuo ambao mwanahabari wetu aliyekuwa online wakati huo aliweza kupiga picha majibu ya Zari yaliyoonesha kumdharau Tanasha pamoja na mtoa zawadi ya simu hiyo, Diamond  au Mondi. “I love my Samsungs they have the best photo quality. iPhone 11 Pro nishafanya order za watoto,” Zari alimjibu Theddy akiwa ana maana kwamba anapenda simu hizo za Samsung ambazo zina picha nzuri na iPhone (aliyopewa Tanasha na Mondi) amewaagizia watoto wake.

POVU LA TEAM  MONDI KAMA LOTE

Baada ya Zari kutoa kauli hiyo nzito ya kuwananga Tanasha na Mondi, wafuasi wao waliibuka kwenye mitandao hiyo na kutoa maneno makali dhidi ya Zari kwa kile walichodai kuwa amewachefua. “Kwendraa huko wewe bwana, simu yetu sisi wewe unawashwa na nini? Tupishe bwana huko.”

“Tatizo unampenda sana Mondi huwezi kufanya mambo yako bila kumuongelea? Kweli nimeamini Mondi ni kama maji, usipoyanywa utayaoga.” “Unajishaua kwamba una hela mbona kwa muda mrefu uling’ang’ania kukaa kwenye nyumba yetu hapo Sauz?”

Hayo yalikuwa baadhi ya maoni ya wafuasi wa Mondi na Tanasha kwenye komenti za picha hiyo ya Zari. Mashabiki hao walicharuka kama wametiwa ndimu kutokana na kuamini bosi wao Mondi ana hela, hivyo kuambiwa simu aliyojipinda kumnunulia mpenzi wake kama zawadi, yeye anawanunulia watoto ni dharau isiyokuwa na mfano.

Risasi Jumamosi lilizungumza na mtu wa karibu wa familia ya Mondi kuhusu dharau hiyo waliyoonyeshwa na Zari, ambapo alieleza jinsi walivyoipokea kwa masikitiko na kusema wanamuandalia jambo kubwa na zito.

“Ye si katuvua nguo kwamba sisi hatuna hela na kwamba simu ambayo Diamond amempa Tanasha yeye anawapa watoto wachezee sijui, kuna jambo tutamfanyia na sisi we ngoja utaona,” alisema mtu huyo. Alipotafutwa mama Diamond, Sanura Kassim pamoja na Mondi mwenyewe, simu zao ziliita bila kupokelewa.

KUMBUKUMBU YA VITA

Hii si mara ya kwanza, Zari na familia ya Mondi wanaingia kwenye vita ya maneno. Mara kadhaa tangu Mondi aachane na Zari, Februari 14, mwaka jana wamekuwa wakirushiana maneno ya hapa na pale ambapo familia ya Mondi imekuwa ikijibu mashambulizi kuonesha kwamba si wanyonge!

Comments are closed.