The House of Favourite Newspapers

Kwa Heri Mngereza, Mlezi wa Sanaa Tanzania

0

Viongozi mbalimbali wa kitaifa wakiongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa, wameungana na waombolezaji wengine kuanga mwili wa aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mngereza.

Zoezi hilo linafanyika leo Disemba 29, 2020, katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es salaam. Mbali na viongozi lakini wasanii na makundi mbalimbali ya sanaa wamefika kumuaga.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza alifariki dunia usiku huu wa Disemba 24, 2020, akiwa hospitali jijini Dodoma.

 

 

 

 

Leave A Reply