The House of Favourite Newspapers

KWA HILI LA MAKOSA YA MTANDAO; MASTAA MTAPATA TABU SANA

KILA kukicha, wapo mastaa ambao wamekuwa wakijiachia kihasara mitandaoni bila kujali kwamba wanaenda kinyume na maadili ya Kitanzania na wao ni kioo cha jamii ila sasa muarobaini wao umepatikana hivyo wakiendeleza tabia hizo, hakika watapata taabu sana.

Wapo mastaa ambao wamekuwa ni sikio la kufa kwani licha ya kuwaona wenzao wakipewa adhabu ya kufungiwa kufanya sanaa, bado wamekuwa wakiweka picha au video za nusu utupu au za kimahaba ambazo huwa ni kero kwa jamii inayowazunguka.

Risasi Mchanganyiko lilipata nafasi ya kuzungumza na msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania (ACP), Barnabas Mwakalukwa ambaye alifafanua na kusema kwamba kutokana na vitendo hivyo kushamiri hasa kwa wasanii, wamekuwa wakitoa elimu

Taifa (Basata), vyama vya wasanii pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwamba waache kwani ni kosa kisheria.

Aliendelea kusema kwamba wamekuwa wakitoa elimu juu ya sheria ya mtandao kwa wasanii mbalimbali na baada ya hapo utekelezaji wa sheria ikiwa ni pamoja na kuwakamatwa, kuwapeleka mahakamani au kuwatoza faini.

WATAPATA TAABU SANA!

ACP Mwakalukwa aliendelea kusema kwamba mastaa au wasanii ambao watakwenda kinyume na sheria ya mtandao watapata tabu sana kwani sasa hivi kuna kitengo maalum kinachofanya doria mitandaoni kwa kufuatilia wale ambao wanavunja sheria ya mtandao kwa kuposti picha chafu.

“Sheria ya mtandao inakataza kuposti picha chafu maana hilo ni kosa la jinai, tumekuwa tukitoa elimu sana kwa wasanii kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, pia Baraza la Sanaa la Taifa na vyama vyao hivyo baada ya hapo sheria itafanya kazi yake.

“Endapo mtu au msanii ataposti picha chafu atakamatwa na kupandishwa mahakamani ambapo adhabu yake itakuwa ni kwenda jela au kupigwa faini hivyo wasanii wawe makini na hilo,” alisema ACP Mwakalukwa.

AWAPA SOMO MASTAA

Kwa upande mwingine kamanda huyo aliwapa somo mastaa kutambua kuwa sanaa siyo kuposti picha za ngono, kucheza uchi au kuvaa vimini (nusu utupu) bali ni kazi kama zilivyo nyingine hivyo kwa kuwa wao ni kioo cha jamii wanatakiwa kuwa mabalozi wazuri kwa kuheshimu utamaduni wa nchi ya Tanzania.

“Mastaa wa sanaa mbalimbali wanatakiwa kuangalia utamaduni wa nchi kwani msanii mzuri ni yule ambaye haposti picha chafu hivyo ili kuondokana na kashikashi za kukamatwa na kupandishwa mahakamani, wanatakiwa kusoma sheria ya makosa ya mtandao na kuacha kuposti picha chafu,” alimaliza ACP Mwakalukwa.

TUJIKUMBUSHE

Mastaa mbalimbali wamekuwa wakiachia video na picha chafu mitandaoni huku nyingine zikiwa ni za mahaba, hali ambayo inawachefua na kuwakera wanajamii ambapo hivi karibuni msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ video yake akiwa anacheza na mwanaume kihasara jukwaani ilivuja na kuzua gumzo.

Wasanii wengine ni Vanessa na Jux ambao waliachia picha ikiwaonyesha wakinyonyana ndimi jukwaani huku mashabiki wakiwashuhudia, mwingine ni Nandy na Billnas ambapo video yao wakiwa faragha ilivuja na baadaye kuitwa na Basata ambapo Nandy aliwaomba msamaha mashabiki wake.

Wengineo ambao wamekuwa na tabia hizo ni mwanamuziki Mbosso, Uwoya aliyeachia picha akiwa amevaa gauni lililokuwa likimuonyesha umbile lake lilivyo ambapo baadaye alijitetea kuwa alikuwa ufukweni na wengine wengi

STORI : NA GLADNESS MALLYA

Comments are closed.