The House of Favourite Newspapers

Kwa Nini Uzaliwe, Uishi, Na Kufa Tu!

mentalgetty4

Karibu mpenzi mdau na msomaji wa makala za ujasiriamali, katika somo letu ambao lina lengo la kukujenga na kukufanya uweze kujitambua katika maisha yako.

Maisha ni safari ndefu sana ambayo ina misukosuko mingi sana na kama usipokuwa makini unaweza kujikuta ukikata tamaa na kuchukua maamuzi magumu.

Mungu si wa hivyo kama ambavyo unadhani, kuwa amekuleta duniani uteseke, amekuleta uishie kuishi, kufa na kutoweka, la hasha! Bila shaka kuna kitu muhimu sana katika maisha yako kakiweka ndani yako ila wewe hujakifahamu, hujakigundua.

Nafahamu ugumu uliopo katika jamii yetu kugundua au kubaini uwezo ambao umepewa na mwenyezi Mungu, ukipata muda mzuri wa kujiuliza kuwa ‘hivi ni kweli nimezaliwa kuteseka, kuishi kwa kuteseka pengine hata kifo change kiwe ni cha mateso’ kama ndiyo nililetwa duniani nifanye nini? Niteseke, kama hapani ni kwa nini kila siku maisha yangu yamekuwa ni ya machungu, kila kukicha mimi ni mtu wa majanga.

Ukipata muda wa kutafakari mambo hayo na mengine mengi kwa kila nina akika utasimama tena na kuwa imara huku tayari ukishakuwa umebaini uwezo ambao Mungu ameuweka ndani yako.

Ni imani yangu mwanadamu hajaumbwa kuishi na kufa bila kaucha kitu chochote duniani kama kumbukumbu ya maisha yake, ingaw akumbukumbu hizo zinaweza kuwa mbaya kama farao au nzuri kama Nelson Mandela.

Kikubwa ni kujichunguza vizuri kuwa wewe umezaliwa kufanya nini na hakika siku ukijua ulichozaliwa kukifanya na ukafanikiwa kukifanya utakuwa umeishi maisha mazuri na yenye furaha sana hapa duniani, kwani umeishi maisha ambayo uliletwa uyaishi.

Ninahisi wewe ndiye amani ya nchi baadhi zenye machafuko duniani ila hautaki kujiamini, kuchukua hatua na kuthubutu. Yawezekana wewe ndiyo mfumo rahisi na mwepesi zaidi wa mawasiliano duniani ila haujafahamu.

Basi imetosha sana kuishi hivyo ambavyo unaishi kwa sasa, jipange upya na uchukue hatua ya kutoka hapo ulipo na kuelekea ambapo unastahili kuwepo.

Kwa ushauri na maoni tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook, Insta: mimi_na_uhusiano, Twitter:mimianauhusiano au jiunge na M&U WhatsApp kwa Na. 0657486745 kupata mengi zaidi.

NIKUTAKIE SIKU NJEMA NA MUNGU AKUBARIKI SANA.                       

Comments are closed.