The House of Favourite Newspapers

Kwa Tshabalala, Huyu Kwasi Anasubiri

BAADA ya kushindwa kung’ara msimu uliopita kama ilivyokuwa kwa msimu huu na kuishia kusugua benchi, nahodha msaidizi wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ amesema bidii yake mazoezini imemfanya kocha Patrick Aussems ampe shavu.

 

Msimu wa mwaka 2016/17 beki huyo aliibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara baada ya kuwashinda Simon Msuva na Aishi Manula lakini msimu uliopita hakuwa na nafasi ndani ya kikosi hicho kikiwa chini ya Mfaransa Pierre Lechantre.

 

Kikosi cha Simba kwa upande wa mabeki wa kushoto imekuwa ikiwatumia wachezaji wawili ambao ni Tshabalala na Asante Kwasi na msimu uliopita baada ya Kwasi kusajili dirisha dogo Tshabalala hakuwa na nafasi tena mpaka msimu huu ulipoanza.

Akizungumza na Spoti Xtra, Tshabalala alisema; “Kila mtu anapata nafasi yake kutokana na bidii zake mazoezini ndiyo imekuwa chachu ya mafanikio kwangu sababu kujituma mazoezini ndiyo kumeweza kumshawishi kocha na akanipa nafasi ndani ya kikosi chake bila tatizo lolote ingawa tuko wengi.”

 

“Kwa msimu uliopita unaweza kusema siku na bahati au haikuwa nafasi yangu mimi kuweza kuonekana lakini safari hii nafasi hiyo imeonekana na mimi nazidi kupambana kuhakikisha naendelea kufanya vizuri kwa kuwa bidii ni jambo la muhimu na kukufanya ufanikiwe na sio kitu kingine,” alisema Tshabalala

MARTHA MBOMA

Comments are closed.