LICHA YA MKWARA WA BASATA… GIGY SIKIO LA KUFA – VIDEO

LICHA ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kukemea wasanii kila kukicha kuacha kukaa nusu utupu, staa wa muziki wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amegeuka sikio la kufa.  

 

Gigy alithibitisha hilo kwenye Tamasha la Wasafi Festival lilifanyika usiku wa Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Tamasha hilo ndiyo mara ya kwanza kufanyika nchini likiandaliwa na Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) chini ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

 

Taarifa ikufikie kuwa Gigy alikuwa ni mmoja wa wasanii waliokinukisha ambapo baada ya kupanda jukwaani mashabiki wengi walipandwa na mzuka walipomuona. Gigy alifanya ‘laana’ ya aina yake jukwaani ambapo alikuwa amevalia kivazi ambacho kina mpasuo mkubwa kuanzia kiunoni mpaka miguuni huku akiwa uchi kwani hakuvaa nguo ya ndani ‘kufuli’ hali iliyozua gumzo kwa mashabiki wake.

 

Licha shangwe za kutosha kutoka kwa mashabiki huku akirusha miguu juu na kubaki uchi kabisa kuanzia kiunoni kushuka chini, wengi wa mashabiki hao hasa wanaume wakware walionekana kugombania kusogea eneo la mbele ya jukwaa kumchungulia ambapo Gigy alikuwa akiinama mara kwa mara akiimba wimbo wake wa Papa na nguo hiyo kuacha nyeti zake nje.

 

“Yaani huyu Gigy ni sikio la kufa maana kila siku Basata wanawakemea wasanii waachane na kuvaa nguo zisizokuwa na maadili, lakini angalia alichovaa, kwa kweli anatia aibu,” alisikika dada mmoja akijadili na mwenzake.

 

Kutokana na kunogewa na kumpiga chabo, Gigy ulipofika muda wa kushuka jukwaani mashabiki hao huku wakiendelea kumpiga chabo walisikika wakisema: “Asishuke huyu, DJ unatubania, mwache aendelee.” Hata hivyo, alimaliza kuimba na kushuka jukwaani japokuwa mashabiki walikuwa wakiendelea kumgombea.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Basata kupitia Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza ilimtaka Gigy kuripoti ofisini kwa Naibu Waziri huyo baada ya kuhusika na kutupia picha za nusu utupu mitandaoni akiwa sambamba na mwanamitindo, Jane Rimoy ‘Sanchi’.

LOOH! GIGY Apanda UCHI Stejini / Wasafi Festival Moro

Toa comment