The House of Favourite Newspapers

Linex MUZIKI NA TUMBAKU NDIYO MAISHA YANGU

Sunday Mjeda ‘Linex’.

 

UKITEMBELEA katika viunga vya Mkoa wa Kigoma leo, ukauliza watu maarufu wanaopendwa mkoani humo pasi na shaka utajibiwa majina matatu, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, mchekeshaji Baba Levo na mwanamuziki aliyezaliwa katika Wilaya ya Kasulu, mkoani humo, Sunday Mjeda ‘Linex’.

Watu hawa wanapendwa sana Kigoma na kila mmoja kwa sababu zake. Lakini kwa upande wa Linex ni kwa sababu ameitangaza vyema lugha ya kabila la Waha, wanaopatikana katika mkoa huo, ambapo kwenye nyimbo zake kadhaa amekuwa akitumbukiza misemo na maneno kutoka katika kabila hilo.

 

Staili hiyo ya kutumia lugha yake mama ndiyo imemfanya pia Linex, kuwa tofauti na wanamuziki wengi Bongo, amewahi pia kufanya vizuri na ngoma nyingi zikiwemo Mama Halima, Salima, Aifola na Mahakama ya Mapenzi.

Lakini kwa muda Linex amekuwa kimya, ambapo Showbiz Xtra, imeamua kumuibukia na kupiga naye stori mbili tatu. Msikie;

 

Showbiz: Bado tu unapika kazi mpya kaka, maana kila mara unatuambia unapika na kazi hizo haziivi?

Linex: Ha ha haaa! Zimekwishaiva tayari. Nina kazi mbili ninatarajia kuzitoa wiki hii. Moja nimefanya na Young Dee inaitwa Mapito na nyingine inaitwa I’ am Sorry.

Showbiz: Nakuwa surprised kusikia umefanya kazi na Young Dee, bila shaka hii ndiyo kazi yako ya kwanza kufanya na rapa?

 

Linex: Yaa ni kweli. Sijawahi kufanya kazi na rapa yeyote huko nyuma kwa sababu nilikuwa naamini peke yangu nafiti na ninaweza kufanya bora zaidi bila hata kumshirikisha mwanamuziki wa kuchana.

Showbiz: Nini kimetokea sasa mpaka ukaamua kumshirikisha Young Dee?

Linex: Nipo katika maandalizi ya kuachia albamu yangu mpya, kwa hiyo nahitaji mashabiki wangu wapate vitu tofauti-tofauti. Siwezi kufanya albamu peke yangu.

 

Showbiz: Tumeona baadhi ya wanamuziki ambao wametoa albamu hivi karibuni, akiwemo Diamond na Vee Money wamekwenda nje ya nchi kufanya uzinduzi, kwako una mpango wowote wa kufanya kitu kama hicho?

Linex: Sina mpango huo na sihitaji kufahamu hata nini kimewas-ukuma kwenda nje. Nitafanya kile ambacho kwangu nitaona ni bora kufanya.

Showbiz: Hii itakuwa albamu yako ya ngapi kufanya?

 

Linex: Albamu ya pili, ya kwanza ilikuwa ni Mama Halima na ilifanya vizuri kwa mauzo.

Showbiz: Mbali na kazi ulizofanya, Linex ni kama ulikuwa umepotea kidogo, nini tatizo?

Linex: Kila biashara ina kupanda na kushuka. Mimi ni mfanyabi-ashara wa muziki, kwa hiyo suala la kupanda na baadaye kushuka ni sehemu ya matokeo kwenye kazi yangu.

Showbiz: Kuna taarifa zilivuma hivi karibuni kwa-mba um-eoa na ume-funga ndoa, kuna ukweli juu ya taarifa hizi.

 

Linex: Si kweli. Sijaoa na ikifika nika-fanya kitu kama hicho bila shaka mas-habiki wangu watapata taarifa kwa sababu mimi ni maarufu na hakutakuwepo mambo ya tetesi.

Showbiz: Mbali na muziki kwa sasa unajishughulisha na nini?

Linex: Ninajishughulisha na kilimo cha tumbaku. Ukweli ni kwamba tumbaku na muziki ni kila kitu kwangu, kwa hiyo nikiwa sisikiki basi nipo mashambani ninakomaa na tumbaku.

 

Showbiz: Nakushukuru sana Linex, pengine kama una lolote kwa mashabiki wako?

Linex: Bado ninahitaji sapoti yao. Kiukweli bila mashabiki muziki wangu si kitu, kwa hiyo wazidi kunipa sapoti. Na hata nichukue nafasi hii kuwashukuru Global, mmekuwa nami kabla sijafahamika na mara kwa mara mmekuwa mnanipa sapoti. Shukrani pia.

Showbiz Xtra.

Comments are closed.