The House of Favourite Newspapers

FT: AZAM FC 1-2 YANGA KUTOKA AZAM COMPLEX

 MPIRA UMEKWISHAAAAAA

DAKIKA 3 ZA NYONGEZADk 90, Mahadhi anaipangua difensi ya Azam na kuachia mkwaju safi wa krosi lakini hakuna mtu katika nafasi
Dk 85, Yanga taratibu wanaanza kupoteza muda huku Azam FC wakiwa hawataki kupoteza hata senti ya muda
Dk 83, krosi nzuri ya Agyei, Mbaraka anaunganisha vizuri mbele ya Yondani, unatoka kidogo kabisa nje ya lango la Azam
KADI Dk 78 Morris naye analambwa kadi ya njano kwa kumrukia mgongoni Chirwa, inaonekana undava sasa umetawala zaidi
KADI Dk 76 Yondani naye analambwa kadi ya njano kwa kucheza kibabe dhidi ya Mbaraka na Agyei
KADI Dk 75 Tshishimbi analambwa kadi ya njano kwa ubabe, ni kadi ya kwanza ya YAnga leo na ya nne katika mchezo wa leo
SUB 68 Yanga wanamtoa Ajibu, nafasi yake inachukuliwa na Mahadhi
Dk 67 Himid Mao anajaribu mkwaju hapa lakini unakwenda nje
Dk 63, Azam ni zamu yao, lakini mpira wa Chilunda unawahiwa na Yondani, anaondosha hatari
Dk 62, Chirwa anajaribu kuingia vizuri lakini Morris anamdhibiti

Dk 60, Martin anawatoka mabeki wawili wa Azam, anagongeana na Ajibu vizuri lakini kipa Abarola anakuwa mjanja
Dk 57 Agyei katika nafasi nzuri kabisa, lakini anapiga shuti kuuubwa, goal kick
Dk 51 sasa, bado mpira unachezwa muda mwingi zaidi katikati ya uwanja na hakuna timu iliyofungua mipango bora kupata bao la kuongeza au kusawazisha
Dk 51 sasa, bado mpira unachezwa muda mwingi zaidi katikati ya uwanja na hakuna timu iliyofungua mipango bora kupata bao la kuongeza au kusawazishaDk 49, Kangwa anamtoka tena Kessy na kumimina krosi safi kabisa, goal kick
Dk 46, Chirwa anawekwa chini na Nkongo anasema ni madhambi. Anaupiga vizuri Gadieal na Yanga wanaonekana kama wameanza kwa kasi nzuri
Dk 45, Yanga ndiyo wanaanza na kujaribu shuti lakini ni dhaifu

MAPUMZIKO
DAKIKA 2 ZA NYONGEZAGOOOOOOOOOO Dk 44, shuti kali la Gadiel Michael linakwenda moja kwa moja wavuni baada ya kumshinda kipa wa Azam FC
KADI Dk 43 Kingu naye analambwa kadi kwa kumuangusha Makapu
Dk 42, shambulizi jingine zuri la Yanga lakini Razak anadaka vizuri mkwaju wa faulo wa Martin
Dk 39 Kangwa anamgongea mpira Kessy na kuwa kona, inachongwa tena na Kangwa inakuwa haina faida
SUB Dk 36, Azam FC wanamuingiza Salim Hoza kuchukua nafasi ya Benard Arthur
Dk 36 Azam FC anatoka Bernard ingia Salmin Hoza. Azam FC 1-1 Yanga SC
Dk 35, Martin anajaribu vizuri hapa, mpira wake unatoka juu kidogo ya lango la Azam  FC
GOOOOOOOO Dk 30, Ajibu anatoa pasi nzuri kabisa kwa Chirwa anayeuwahi mpira mbele ya kipa wa Azam na kuukwamisha wavuni kwenye nyavu zilizo wazi
Dk 28, Ajibu akiwa mbali anajaribu vizuri kabisa, lakini kipa Abarola yuko makini kabisa
Dk 26, Azam FC inabidi wajihadhari kutokana na kucheza faulo nyingi mfululizo
Dk 24 Kessy anakwatuliwa na Kangwa mbele ya mwamuzi wa akiba, lakini anaonekana kama hakuona. Yuko nje anatibiwa


KADI Dk 22, Sure Boy analambwa kadi kwa kumuangusha Martin


Dk 20, Yanga bado wako katika lango la Azam, wanagongeana vizuri lakini Ajibu anapiga juu na kuwa goal kick
Dk 19, Yanga wanafanya shambulizi jingine zuri, Tshishimbi anagongeana na Ajibu na Chirwa anaachia mkwaju unatoka pembeni kidogo
Dk 17, Kangwa tena, anaingiza krosi nyingi nzuri, Yondani anaruka na kupiga kichwa anaondosha
Dk 16 Kangwa anamzidi tena ujanja Kessy, anaingiza krosi safi hapa, Yanga wanaokoa
Dk 15, Yanga wanagongeana vizuri kabisa, Tshishimbi anaachia mkwaju matata kipa Azam anadaka na kutema, lakini anauwahi tena


Dk 12, shambulizi jingine pole la Azam FC, Arthur anaachia mkwaju hapa lakini ni chakula kwa Rostand
KADI Dk 10, Chilunda anamkwatua Kessy na mwamuzi Nkongo anamramba kadi ya njano ya kwanza katika mechi ya leo Dk 7, Yanga tena, pasi nzuri ndani ya 18, lakini Tshishimbi anachelewa
Dk 5, Ajibu anajaribu mkwaju hapa lakini unakuwa dhaifu kabisa
GOOOOOOOOOO Dk 3, Kangwa anamtoka Kessy, anamtoka Raphael Daud na kuingiza krosi safi kabisa, Iddi anaunganisha na kuandika bao la kwanzaDk 2, Kessy anachuana vizuri na Kangwa na kumzidi maarifa, inakuwa goalkick
Dk 1, Yanga wanaanza na kufika katika lango la Azam FC, wanaokoa, nao wanaanza kushambulia kwa kasi
 
 
TAKWIMU ZAO KABLA YA LEO…
Zimekutana 31
Yanga shinda 12
Azam shinda 11
Sare 8

Yanga ilifunga mabao 41
Azam FC ilifunga mabao 40

Comments are closed.