Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga na mwandishi wa habari, Muhingo Rweyemamu aliyefariki dunia Jumamosi iliyopita, Septemba 2 anaagwa leo jijini Dar es Salaam.
Katika utumishi wake, Muhingo Rweyemamu aliwahi pia kuwa mkuu wa wilaya za Morogoro, Makete na Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited.

