Naibu Waziri Masauni Atoa Kauli kwa Madereva Kupunguza Ajali (VIDEO)

Naibu Waziri Hamad Masauni akizungumza wakati wa Tamasha hilo.

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Eng. Hamad Masauni amewaasa madereva wa magari na pikipiki kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali na vifo visivyo vya lazima.

Rais Mstaafu, Mzee Ally Hassan Mwinyi akitoa nasaha kwenye tamasha hilo.

 

Akizungumza wakati wa hitimisho la Tamasha la Usalama Barabarani lililofanyika leo katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar, Masauni amesema kila kijana ana wajibu wa kuhakikisha anazijali sheria za barabarani ikiwa ni pamoja ma kuvaa kofia ngumu kwa waendesha bodaboda na kuepuka kupanda mishkaki (zaidi ya abiria mmoja) kwenye pikipiki moja.

Wananchi wakijumuika.

“Kila mtu anapotoka hapa atoke kitu kichwani mwake, hakikisha unakuwa balozi mzuri wa kupunguza ajali barabarani. Sizani kama utatoka hapa leo halafu bado upande mshkaki, au upande pikipiki bila helmet, sote tuwe watiifu wa sheria zetu za barabarani ili kuepusha ajali zisizo za lazima.

Wananchi waliohudhuria tamasha hilo.

 

“Ndiyo maana tumewahusisha zaidi vijana kwa kuwa nyie ndiyo wahanga wa hili, madereva wengi ni vijana hivyo ni lazima tuwape elimu hii ili iwasaidie,” alisema Masauni.

Na Hilaly Daudi | Global TV Online

 


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Loading...

Toa comment