Karia: Siwezi Kuifanyia Mabaya Yanga, Nimewasaidia Sana – Video
KWA mara ya kwanza, leo Juni 03, Rais wa TFF, Wallace Karia, ametembelea ofisi za Global Group na kufanya mahojiano na Global Radio kuhusiana na masuala mbalimbali ya mpira nchiini.
Miongoni mwa mambo aliyoyasema Karia ni haya; “Nilivyokuwa naisikia Global na nilivyoiona ni tofauti sana, ni kubwa sana. hongereni sana. Sisi tulikuwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wakati wa FAT, mkutano wetu ndio uliyopitisha mabadiliko ya kwenda TFF, sisi ndio wanaharakati tuliomuingiza Mzee Tenga kuwa Rais wa TFF.
“Katika maisha yangu mimi nilijiwekea kwamba lazima nipunguze watu wa kunipa maelekezo, hili iliendana na utendaji wangu. Kuna siku nilimwambia Mzee Tenga kwamba kila siku Timu yetu ya Taifa inafungwa, kwa nini tusipeleke tu vijana tukawaamini, hata tukifungwa sawa, lakini tutakuwa tumejificha humo lakini tutakuwa tumewapa exposure.
“Good Governance ans Admiration…. kuhusu adhabu kali sisi tunafuata kanuni tulizozichukua FIFA, huwezi kuweka adhabu ndogo watu watakutukana kila siku kwa sababu wanaweza kulipa faini.
“Ligi yetu imepanda hadhi tangu tuingie madarakani, tumekuwa wa nane Afrika, tumewazidi Nigeria na Algeria licha ya kwamba tukicheza nao Timu ya Taifa kupata matokeo imekuwa ngumu. Azam TV na TBC ndio waliingia kwenye kuwania dili la kutangaza Ligi Kuu kwenye Televisheni na Radio.
“Ukienda mtaani utasikia watu watakwambia hakuna Rais wa TFF aliyeionea Yanga Sc kama Karia, lakini ukienda ndani ya TFF watakwambia hakuna mtu aliyeisaidia Yanga kama Karia, kama mkiwapata viongozi wasema ukweli, watawaambia.
“Baada ya Manji kupata matatizo na kuondoka, Yanga ilipita katika wakati mgumu, nimeshirikiana na Sanga kuisaidia Yanga. Mimi ni Coastal si Yanga, walikuwepo Tenga amecheza Yanga, Malinzi alikuwa Katibu Mkuu wa Yanga lakini hawakuifanyia Yanga kama nilivyofanya mimi.
“Siwezi kuifanyia mabaya Yanga, hizi ni timu zinazoililetea heshima Taifa, mimi ninaheshimiwa huko nje kwa sababu ya Simba na Yanga. Sisi wenyewe hatutambui ukubwa na heshima wanaotupa hawa mabwana kwenye ukanda wetu huu, hizi timu naziheshimu sana.
“Suala Asukile alizungumza akaitwa na Kamati. Suala la Kabwili lilikuwa la muda mrefu na nje ya Mchezo, Yanga walisema lipo TAKUKURU ndio wanahusika na uchunguzi, alisema mpaka alipigiwa simu mimi siwezi kwenda kuuliza watu wa mitandao, ni kazi ya TAKUKURU,” amesema Karia.