The House of Favourite Newspapers

Makonda Amtaka Mkandarasi Akabidhi Jengo la Hospitali – Video

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo Oktoba 16 ametembelea na kukagua ujenzi wa jengo la ghorofa tano la Mama na Mtoto Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala na kumtaka mkandarasi wa jengo hilo kutoka Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kuongeza kasi na masaa ya kazi ili akabidhi jengo hilo kabla ya Desemba 30, mwaka huu.

Amesema ujenzi wa jengo hilo ulisimama tangu mwaka 2014 lakini  Rais John Magufuli aliamua  kutoa zaidi ya Shilingi Billion 2.1 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo ili kupunguza kero kwa wananchi.

Aidha amesema jengo hilo litaanza kutumika mwezi Januari mwakani ambapo ndani yake litakuwa na uwezo wa kuchukua vitanda 100 vya Mama na Mtoto na fedha ya kununua vifaa tiba ipo tayari.

Pia amesema mbali na ujenzi wa huo  serikali inaendelea na ujenzi wa Hospital ya Wilaya Mabwepande na tayari upo kwenye hatua za kujenga Kituo cha Afya Kawe na Bunju ambapo miradi yote ikikamilika itasaidia kumaliza changamoto za Afya Wilaya ya Kinondoni.

 

Comments are closed.