The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Azindua Ujenzi wa Maghala ya Chakula na Vihenge – VIDEO

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Kassim Majaliwa ameweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Maghala ya Chakula na Vihenge mjini Dodoma leo Jumamosi, Aprili 21, 2018.

 

“Mradi huu wa maghala ya nafaka unalenga kuhakikisha kunakuwepo na upatikanaji wa chakula cha kutosha pamoja na kupunguza upotevu wa chakula unaosababishwa na uhifadhi mbovu. Sasa tutafungua milango ya masoko ya ndani na nje ya nchi ili kuwezesha wakulima wetu kujipatia fedha kupitia kilimo, pia lazima tujiridhishe kuwa tunacho chakula cha kutosha kila mwaka.

 

“Tumeamua kuipa kazi Wizara ya Kilimo chini ya Dkt. Tizeba kuhakikisha wanasimamia kilimo kwa dhati, lakini pia tumeshauri kufanya kilimo kwa kanda. Mwaka jana 2017 tuliziona nchi za jirani zetu hazikuwa na chakula cha kutosha, tukaamua kuzuia kuuza chakula nje ili tusiwauzie malighafi, tulichokifanya badala ya kuwauzia mahindi tukawauzia unga,” alisema  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

 

Naye Waziri wa Kilimo, Charles Tizeba amesema; “Kuanzia sasa mazao ya biashara kama pamba na kahawa yataanza kuuzwa kwa mfumo wa vyama vya ushirika katika msimu huu. Wakulima hawataruhusiwa kuuza mazao ya kahawa na pamba wao wenyewe, watakusanya kwenye vyama vya ushirika ambavyo ndivyo vitakuwa na jukumu la kuuza mazao hayo.”

 

Comments are closed.