The House of Favourite Newspapers

MAAFALI YA 42 SHULE YA MCHANGANYIKO MAZINYUNGU YATIKISA

SHULE  ya Msingi yenye mchanganyiko wa wavulana na Wasichana, Mazinyungu iliyopo wilaya Kilosa mkoani Morogoro hivi karibuni ilifanya mahafaLi ya 42 ya kuwaaga wanafunzi wake 82 waliohitimu elimu ya msingi baada ya kufanya mtihani wa Taifa wa darasa la saba ambapo kati baadhi yao walikuwemo wanaulemavu wa macho na wengine wenye ulemavu wa ngozi.

 

Akizungumza katika mahafaLi hayo, mgeni rasmi Mhandisi Gervas Osward Kondobole alisema kuwa alifarijika kuwa mgeni rasmi katika mahafari hayo kwani ndiyo shule aliyosoma na kupatia elimu yake ya msingi na kwamba anaona kama amerudi nyumbani kurudisha fadhira.

 

 

“Nafarijika sana kuwa mgeni rasmi hapa kwani ndio shule niliyosoma, hivyo kuja kwangu hapa ni kama nimerudi nyumbani eneo lililoanza kunipatia elimu ya msingi hadi kufikia hatua hii niliyonayo leo,” alisema Kondobole.

Akiendelea kutoa shukrani zake injia Kondobole alisema kuwa licha ya kuja mgeni rasmi anatambua changamoto zilizopo katika shule hii hivyo hakuja mikono mitupu ameleta msaada wake kwa wadogo zake wa Mazinyungu.

“Najua kuna tatizo la umeme na kompyuta, hivyo nimewaletea jenereta kubwa ambalo linauwezo wa kusambaza umeme shule nzima pamoja na kompyuta,” alisema Kondobole kabla ya kuvikabidhi.

 

1.Akikaribishwa na wenyeji wake

2 na 3. Akiwa anasaini kitabu cha wageni

4.akionyeshwa baadhi ya mazingira ya shule

5.Akipokewa maelekezo kutoka kwa mwalimu mkuu wa shule ya Mazinyungu

6.Akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu

7.Moja ya mashine ya kutolea photokopi inayotumiwa na walemavu wa macho

8.Maabara inayotumika kwa ajili ya walemavu

9.Akiwa katika meza kuu na baadhi ya waalikwa

10.Kompyuta inayotumika na walemavu

11.Mmoja ya mwanafunzi mwenye ulemavu wa ngozi akipiga ngoma

12.Baadhi ya walimu wenye ulemavu wa macho

13.Akivishwa skafu na mmoja wa maskauti

14.Akikabidhi msaada wa jenereta

15.Akikabidhi msaada wa kompyuta

  1. Akipeana mikono na mmoja wa wahitimu baada ya kusoma risala

17.Akipeana mikono na mwenyekiti wa kamati ya shule mama Chacha

18.Baadhi ya wazazi waliohudhuria mahafari hiyo

Comments are closed.