The House of Favourite Newspapers

MADAI YA KUBANJUKA NA MREMBO DUBAI DIAMOND AANIKA UKWELI

BAADA ya uvumi kuvuma mitandaoni kuwa mkali wa Bongo Fleva na Mkurugenzi wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond’ ‘amebanjuka’ na mrembo aliyefahamika kwa jina la Christina huko Dubai, mkurugenzi huyo ameibuka na kuanika ukweli wa mambo.  Akizungumza na Risasi Jumamosi juzi, Diamond alianza kwa kusema kuwa amechoshwa na kuhusishwa na kila mwanamke anayeonekana kuwa na mama yake au kuwa naye karibu tu watu wanasema ni mtu wake.

Alisema msichana huyo wa Kibongo mwenye maskani yake Dubai, alikutana naye kama mwenyeji aliyekuwa akiwatembeza maeneo mbalimbali kama watu wengine ambavyo wanaweza kwenda nje na kupokelewa na marafiki zao.

“Mimi na msichana huyo tunafahamiana ameonekana kweli na mama yangu na wamejiachia kwenye picha tofautitofauti lakini ifahamike kuwa alikuwa akitupa kampani tu kama mwenyeji na si mapenzi,” alisema Diamond. Diamond aliongeza kuwa alipokuwa Dubai alikwenda kufanya shoo na kuinjoi na familia yake lakini si kutafuta mademu na wala hakwenda na demu yeyote zaidi ya familia yake.

“Huko niliteketeza fedha nyingi ambazo nisingependa kuzitaja lakini nilifanya kwa ajili ya familia yangu kwani mafanikio niliyonayo ni kwa dua wanazoniombea mama yangu na ndugu zangu pia sikufanya kwa ajili ya mwanamke na nisingekataa kuongozana na mrembo huyo kwani alikuwa kama mwenyeji,” alisema Diamond.

Hata hivyo, gazeti hili lilimsaka mwanamuziki Said Seif ‘Nedy Music’ anayedaiwa kutoka na msichana huyo aliyekuwa na Diamond Dubai ambapo alipopatikana, alidai kuwa hamfahamu kabisa. “Samahani mimi simfahamu huyo msichana na hayo madai nashangaa,” alisema Nedy Music ambaye yuko nchini Ghana kwenye Tuzo za Afrimma.

TUMEFIKAJE HAPA?

Awali, madai yaliibuka mtandaoni kuwa mrembo huyo aliwahi kuwa na uhusiano na msanii Nedy Music na sasa amehamishia penzi kwa Diamond jambo ambalo liliibua mjadala mkubwa mitandaoni

STORI: Hamida Hassan na Musa Mateja, Risasi Jumamos

Comments are closed.