The House of Favourite Newspapers

Madawa ya Kulevya Yamuua Kaka’ke Eric Omondi!

KAKA mkubwa wa mchekeshaji maarufu, Eric Omondi, Joseph amefariki dunia huku dawa za kulevya zikitajwa kuwa ndiyo chanzo.  Saa chache kabla ya kifo chake, Eric alimtafuta kaka yake huyo katika Mitaa ya Downton River Road na kumkuta akiwa katika hali mbaya.

 

Akitumia ukurasa wake wa Instagram, Eric aliweka picha ya braza wake huyo akiwa amevalia jezi ya Timu ya Brazili na kuandika;

“Hii siyo picha niliyopaswa kuiweka hapa kaka yangu… lakini nataka kila kijana wa nchi hii (Kenya) aione…Joseph Onyango Omondi amefariki dunia saa tatu asubuhi, nimemkuta Downton. Alikuwa katika tiba ya dawa za kulevya kwa miaka 19. Mungu ailaze roho yake.”

 

Baada ya muda akaweka picha nyingine na kuandika;

“Kama wewe ni kijana na umefuata akaunti ya Insta hii ni yako! Joseph ni kaka yangu wa damu (baba mmoja mama mmoja)…wa kwanza kuzaliwa mimi ni wa pili na watatu ni Irene Omondi na wa mwisho ni Fred Omondi. Joseph amekuwa mtumwa wa dawa za kulevya tangu shuleni, tulijitahidi kama familia tukashindwa.”

NAIROBI, Kenya.

Comments are closed.