Madee Afungukia Ndoa Yake

MEMBA wa Kundi la Tip Top Connection ambaye pia ni Mkurugenzi wa Lebo ya Manzese Music Baby ‘MMB’, Hamad Ally ‘Madee’ amefungukia ndoa yake kuwa hawezi kufunga kwa kufuata mkumbo kisa staa fulani amefunga ila atakachofanya ni kufanya sapraiz siku yoyote kuanzia sasa na kufunga bila kutangaza.

 

Madee anayebamba na Ngoma ya Sema alisema, kwa sasa bado anaangalia lebo yake hiyo iweze kutanuka zaidi na tayari amefanikiwa kwa msanii Gaza na Dogo Janja ambao ‘wameshasimama’.

 

“Ujue suala la ndoa si la kukurupuka tu unaenda kufunga. Ndoa ni kitu binafsi kabisa na ni maamuzi ambayo yanachukulia kwa mara moja huwezi kuwa na uamuzi tena kwa hiyo mimi kama mimi kufunga ndoa ni mipango na familia yangu ambayo siwezi kuiweka wazi lakini muda wowote kuanzia sasa naweza kufunga,” alisema Madee.

 

NA SHOWBIZ, UWAZI

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment