The House of Favourite Newspapers

Madee: Dogo Janja na Irene Uwoya Hawajaachana

Hamad Ally ‘Madee’ (kulia) akiwa na Dogo Janja.

MKONGWE kunako gemu la Bongo Fleva, Hamad Ally ‘Madee’,  amefungukia uhusiano wa msanii mwenzake, Dogo Janja na mke wake staa wa Bongo Movie, Irene Uwoya, akisema wawili hao hawajaachana.

 

Madee ambaye ni baba mlezi wa Dogo Janja amezipiga chini tetesi hizo ambazo zimekuwa zikipamba moto kwenye mitandao ya kijamii.

 

Ameongeza kwamba yeye mwenyewe anashangazwa na taarifa hizo kuzagaa mitandaoni na watu kuongea masuala mengi juu ya ndoa hiyo bila ya kuwa na uhakika.

“Dogo Janja na Irene Uwoya hawajaachana.  Nani amesema wameachana?  Sidhani kama kuna kitu chochote kimewakuta ila ninachojua mimi wapo sawa, hadi dakika hii tunayozungumza na wapo pamoja kabisa,” amesema.

 

Siku za hivi karibuni kumekuwa na tetesi kuwa wanandoa hao wanaelekea kupeana talaka baada ya tetesi kwamba Uwoya kapata danga lenye pesa ndefu.

Comments are closed.