The House of Favourite Newspapers

Madereva Waliotekwa Hatimaye Wawasili Nchini

Madereva wa raia wa Tanzania waliokuwa wametekwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na baadaye kukombolewa na kikosi cha wanajeshi wa nchi hiyo wamewasili nchini leo na kupokelewa na ndugu zao kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere.

Baada ya kuwasili baadhi ya ndugu walishindwa kuzuia hisia zao na kuanza kulia kwa sauti hali iliyofanya eneo zima uwanjani hapo kughubikwa na hali ya majonzi na furaha kutoka pande zote mbili, ndugu na madereva.

Comments are closed.