The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mafuriko Kampeni za Shigongo Bupandwa – Video

0

MAFURIKO ya wananchi wa Kijiji cha Bupandwamhela wakimpokea kijiji hapo mgombea ubunge wa Jimbo la Buchosa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric Shigongo wakati wa mkutano wake jana Jumapili, Oktoba 18, 2020 katika Uwanja wa Mpira wa Bupandwa.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Shigongo ambaye bupandwa ndipo nyumbani kwao amesema; “Nimeamua kuwatumikia kwa sababu nataka kujenga heshima yangu, baadaye miaka 50 hadi 100 watu waseme maisha ya Buchosa ni bora kwa sababu Shigongo aliishi kabla yangu. Mimi ni mtoto wenu, nimekuwa hapa mmeniona na mnanijua.

“Nataka kuwatumikia kwa moyo wangu wote, lazima nilete mabadiliko, na ninawatumia ujumbe wote ambao bado wanaamini kwenye makambi, haya makundi yametuchelewesha sana, hata Mhe. Rais alizungumza pale Nyehunge kwamba hataki kuona mambo ya makabila na makundi ya Buchosa.

“Ninafahamu wapo watu walionipinga wakati wa kura za maoni, ninawasamehe wote, ninawaomba walioniunga mkono, waliopigana usiku na mchana kwa ajili yangu, msiwachukie walionipinga, lazima tuwe kitu kimoja ili tuweze kushinda changamoto zetu, tukigawanyika hatuwezi kushinda.

“Ndugu zangu nitawaongoza, nitakuwa ikama kiongozi wenu na si mtawala, tutajadiliana pamoja changamoto zetu na tutazitatua pamoja.

“Kabla sijawa mbunge nimeomba barabara ya lami, inachongwa kuanzia Sengerema mpaka Nyehunge, nimeomba kivuko kipya kome nimepewa, nimeomba kivuko kingine Maisome nimeambiwa kitawekewa injini mpya mbili, nimekwenda bugoro nimekuta pesa za kuezeka shule zimezuiliwa na halmashauri nimempigia Mkurugenzi simu ameziachia mara moja.

“Mchague Magufuli awe rais wako, mchague Shigongo amwe mbunge wako, mchague Masumbuko awe diwani wako, wale wanaotembea usiku kuwapigia kampeni Chadema wapuuzeni, wazarauni, wana-CCM wa hivyo hatuwataki, akikugongea mlango mwambie achana na mimi,” amesema Shigongo.

 

Wananchi wa Kijiji cha Bupandwamhela ambapo ndipo nyumbani kwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Buchosa kupitia CCM, Eric Shigongo wakimsindikiza Mgombea huyo mpaka nyumbani kwake jana baada ya kumaliza kampeni zake.

 

 

Leave A Reply