The House of Favourite Newspapers

Maisha Magic Bongo na Multichoice Walivyozindua Chaneli ya Filamu za Kibongo

maisha-magic-bongo-1

Wageni waalikwa wakiwa ndani ya nyumba.

maisha-magic-bongo-2

Mzee Chilo (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Dar, Paul Makonda katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi.

maisha-magic-bongo-3

Mama Kanumba (kushoto) na Natasha wakibadilishana mawazo.

maisha-magic-bongo-4

Msanii Rashid Makupa ‘Kupa’ akifurahia jambo na mpiga picha za filamu, Farid Uwezo.

maisha-magic-bongo-5

Wasanii wakongwe, Mzee Chilo na Jengua wakiwa kwenye furaha.

maisha-magic-bongo-6

Msanii wa vichekesho, Joti akiwa kwenye pozi na warembo.

maisha-magic-bongo-7

Msanii Halima Yahaya ‘Davina’ na Mzee Hashim Kambi wakisalimiana.

maisha-magic-bongo-8

Mzee Chilo akipata ‘tumaji twabaridi’.

maisha-magic-bongo-9

Uzinduzi ukifanyika mbele ya Paul Makonda.

maisha-magic-bongo-10

Barbara Kambogi wa Dstv (mbele), Mwakilishi wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Joyce Fisoo na Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, (TAFF) Simon Mwakifwamba (nyuma) wakikatiza jukwaani wakati uzinduzi ukiendelea.

maisha-magic-bongo-11

Muda wa burudani ya muziki ulipofika Bi. Mwenda (kulia) hakujivunga, alijimwaya mdogomdogo na mdada huyu.

maisha-magic-bongo-12

Wageni wa meza kuu wakiwa jukwaani na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda (wa tano kutoka kushoto), baada ya uzinduzi.

maisha-magic-bongo-13

Wageni waalikwa wakiangalia moja ya filamu ya mfano iliyokuwa ikioneshwa.

Maisha Magic Bongo kwa kushirikiana na maprodyuza wa filamu hapa nchini, wameleta mapinduzi kwenye sanaa ya filamu za Kitanzania. Usiku wa kuamkia jana ilikuwa ni full shangwe ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Mliman City jijini Dar wakati Maisha Magic Bongo kwa kushirikiana na Multichoice Tanzania walipozindua rasmi chaneli yao ya (160) Maisha Magic Bongo.  Katika shangwe hizo wageni mbalimbali walialikwa wakiwemo wasanii wa filamu hapa nchini.

HABARI/ PICHA: RICHARD BUKOS / GPL       

Comments are closed.