The House of Favourite Newspapers

MAKAMPUNI MAKUBWA, YENYE NGUVU ZAIDI DUNIANI

1. Industrial and Commercial Bank of China
Benki hii ni kubwa na yenye uwezo zaidi duniani ikijulikana kwa kifupi ICBC na ikiwa na raslimali za zaidi ya Dola tril. 3 na thamani ya masoko ya Dola bil. 215.  Iko sehemu zote isipokuwa Afrika na Antarctica.

2. China Construction Bank Corporation
CCBC ni kampuni la ujenzi la China ambalo liliingia Marekani mwaka 2006 na kuyanunua matawi ya Bank of America yaliyoko barani Asia.  Matawi hayo yana thamani ya sokoni ya Dola bil. 174 tu, lakini nguvu yake ni kubwa.

3. Apple Inc.
NI dhahiri kampuni la Apple Inc. limo katika orodha hii likiwa na thamani ya sokoni ya Dola bil. 415.

4 Toyota
Kuna jiji nchini Japan limepewa jina la kampuni hiyo, wakati hata nchini Ujerumani hakuna mji unaoitwa Mercedes.  Mauzo ya Toyota yalifikia Dola bil. 255.6 na ina wafanyakazi 320,000.

 5 Samsung
Samsung ni kampuni maarufu kwa kuzalisha tevisheni na smart phone, lakini pia linajishughulisha kwa kiasi kikubwa na bima ya maisha, viwanda vikubwa, uhandisi, masuala ya anga za juu, ulinzi, matangazo na ufugaji wa wanyama.

Ni kampuni lenye makao makuu Korea Kusini na utajiri wake ni kiasi cha Dola bilioni 30.

 

 

Comments are closed.