The House of Favourite Newspapers

Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA ahojiwa na Jeshi la Polisi Dar

0

Patric Ole Sosopi (1)

Patric Ole Sosopi (kushoto mwenye gwanda).

Dar es Salaam,

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema Taifa(BAVICHA), Patric Ole Sosopi  leo amehojiwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa tuhuma ya kutoa lugha chafu inayotishia uvunjifu wa amani.

Patric Ole Sosopi (2)Patric Ole Sosopi (mwenye gwanda).

Sosopi alifika kituoni hapo saa 4.10 asubuhi huku  ameambatana na wakili wake Frederick Kikwelo huku wakisindikizwa na wafuasi watano wa  chama hicho.

Akizungumzia suala hilo baada ya kutoka polisi mwanasheria wake alisema mwenyemkiti huyo alihojiwa kwa nusu saa  na alipewa dhamana na jeshi la polisi huku wakiendelea  na upelelezi wao ambapo ukikamilika watakabidhi kwa mwendesha mashtaka kwa ajili ya kupitia ushahidi.

Sosopi alisema baada ya kuhojiwa alielezwa na jeshi la polisi kuwa arudi Julai 18 mwaka huu lakini hawajampa sababu ya msingi ya kurudi siku hiyo.

“Polisi hawajanipa sababu ya msingi ya kurudi Julai 18 mwaka huu,”alisema Sosopi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro alipoulizwa kuhusu alichohojiwa Sosopi, alisema hana taarifa hizo hivyo atafuatiulia

Leave A Reply