The House of Favourite Newspapers

Makamu wa Rais Akabidhi Misaada ya Futari, Atembelea U-DART

0

1.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samiah Hassan akijiandaa kukabidhi vyakula vya futari. Aliyeko kushoto ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.

2.

  …Akisalimiana na mmoja wa watu wenye mahitaji maalum katika ofisi za U-DART Jangwani jijini Dar.

3

 …Akisoma taarifa iliyokuwa imeandaliwa.

4

 Akitoka ndani ya basi la mwendo wa haraka baada ya kulipanda na kuangalia ubora wake.

5.

Gari la Makamu wa Rais, Samiah Hassan likimsubiri.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samiah Hassan,  amekabidhi msaada wa vyakula vya futari kwa makundi mbalimbali ya watu wenye mahitaji maalum wakiwemo yatima na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.

Hafla hiyo imefanyika jana katika ofisi za U-DART Jangwani jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika utoaji msaada huo, Samiah aliishukuru kampuni ya U-DART na wadau wengine waliotoa msaada huo kwa Waislamu kwa ajili ya futari ya mwezi mtukufu wa Ramadhan na akatumia fursa hiyo kuwaomba watu wengine wenye uwezo kujitokeza kutoa msaada katika kipindi hiki cha mfungo.

Vyakula hivyo vilivyokabidhiwa ni, sembe, mchele, tambi, tende, mafuta ya kula na majani ya chai, sukari na unga wa ngano ambapo makamu wa rais huyo aliwataka kuhakikisha makundi yaliyolengwa kupatiwa msaada huo uwafikie pasipokuwa na mzunguko.

Vilevile alikagua mabasi ya mwendo wa haraka yanayomilikiwa na U-DART ambapo alisema yatasaidia kuwapunguzia wananchi adha ya usafiri  jijini Dar es Salaam.

Naye Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Simon Group aliyekuwa miongoni mwa waliotoa vyakula hivyo,  alivitaja baadhi ya vituo vitakavyopata msaada huo kuwa ni Safina- Mbagala Nzasa, Mwandariwa-Boko, New Hope Group, Hiyari Ophans Centre Chang’ombe, Al-Madina Tandale, Hisani Mbagala Maji Matitu, New Life- Kigogo na Mwana Mbagala kwa Mangaya.

PICHA: SALUM YASIN NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply