The House of Favourite Newspapers

Makamu wa Rais Atoa Rai kwa Wafanyabiashara Kuzalisha Bidhaa Zenye Uhitaji Mkubwa Nchini

0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Isdor Mpango akiongea katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango ametoa rai kwa wafanyabiashara nchini kuwekeza nguvu zao katika kuzalisha biadhaa ambazo zina uhitaji mkubwa nchini.

Wageni waalikuwa, Wafanyabiashara pamoja na Wananchi wakisikiliza Hotuba ya Makamu wa Rais Dkt, Philip Mpango

Dkt Mpango ameyasema hayo wakati akizindua maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam  yaliyofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam ambapo amesisitiza bidhaa kama mafuta ya kupikia, Sukari, Unga wa Ngano pamoja na bidhaa za Ujenzi kama Mabati, Nondo pamoja na Saruji.

 

Aidha amewaasa Watanzania kuunga mkono juhudi za Wajasirimali wazawa kwa kupenda na kujivunia bidhaa zinazozalishwa nchini kwani itasaidia kutengeneza ajira, kukuza pato la mtu binafsi pamoja na pato la Taifa kwa ujumla.

Leave A Reply