The House of Favourite Newspapers

Makazi Mapya Ya Angelina Jolie Haya Hapa

jolie-16Chumba cha kulala wageni.jolie-1Ukumbi mdogo.jolie-2Chumba maalum cha mazoezi.

jolie-3Chumba cha kulala Angelina Jolie.jolie-4Chumba cha kupumzika wageni.jolie-5Pembezoni mwa bwawa la kuogelea.jolie-6jolie-7Sehemu ya chakula.jolie-8jolie-10sebule.jolie-11Bwawa la kuogelea. jolie-13 jolie-15Mwonekano wa nje wa nyumba hiyo.

NEW YORK MAREKANI: Gumzo kubwa ulimwenguni kwasasa kwenye masuala ya burudani ni kuachana kwa wanandoa maarufu  Angelina Jolie na Brad Pitt.

Baada ya wawili hao kutalakiana, Angelina Jolie sasa anahamia kwenye mjengo uliopo pembezoni kabisa mwa Malibu  huku akiondoka na watoto wake wote, ambao jumla yao wako sita.

Kwenye nyumba hiyo ya kifahari, Angelina atakuwa akilipa kodi $95,000 kwa mwezi (zaidi ya shilingi milioni 209 kwa mwezi).

Inadaiwa kuwa muigizaji huyo alipanga kwenye nyumba hiyo yenye thamani ya $12m, wiki tatu kabla ya kudai talaka toka kwa Pitt.

Ina ukubwa futi za mraba, 4,409, ikiwa na vyumba vitano na mabafu matano na itatumiwa na yeye na watoto wao, Maddox, 15, Pax, 12, Zahara, 11, Shiloh, 10, mapacha Vivienne na Knox, 8.

Jolie na Pitt walianzisha uhusiano mwaka 2004 wakati wakishoot filamu ya Mr. & Mrs. Smith, wakati huo Brad alikuwa amemuoa Jennifer Aniston kabla ya kuachana naye na kumuoa Jolie.

 

Comments are closed.