The House of Favourite Newspapers

MAKONDA ALIVYOKUTANA NA WAJANE LEO (PICHA +VIDEO)

Makonda akizungumza na wajane.

Umati wa wajane leo ulifurika kwenye mkutano walioitwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda uliofanyika Ukumbi wa Mlimani City Dar kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.

Katika kile kilichooneakana wajane wengine kuwa na changamoto nyingi Makonda alisema matarajio yake yalikuwa kupokea wajane elfu tatu lakini umati uliofurika ulimshangaza na kumhuzunisha.

Shigongo akiwapa wajane hao maarifa ya kuishi maisha bora.

Akizungumza na wajane hao Makonda alisema jukumu alilopewa na Rais Dk. John Pombe Magufuli ni kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi wa Dar hivyo atafanya kama alivyoagizwa na kusema wanaombeza kwa kuanzisha mambo na kuyaachia hewani waache waandelee kusema hivyo.

Katika mkutano huo Makonda aliwapa nafasi wanasheria kuwafafanulia sheria mbalimbali haswa za mirathi ambapo wajane wengi wamekuwa wakidhulumiwa kutokana na kutozifahamu.

Makonda akisalimia na Shigongo baada ya kumaliza kuwapa somo wajane.

Katika kilichoonekana wanawake hao kupata ufahamu walionekana kushangilia kwa mayowe na kushangilia kila walipoguswa na mambo ambayo hawakuyafahamu.

 

Pamoja na kunolewa kisheria wajane hao walipata mafunzo ya kiujasiriamali kutoka kwa Mkurugenzi wa Global Group, Eric Shigongo aliyewafundisha jinsi wa kutumkia kipato kidogo walichokuwa nacho.

 

Shigongo aliwatolea mfano wa mjane anayetumia kipato kidogo alichonacho kununua pea kumi za viatu na rudo madera badala ya kutumia kipato hicho kuwekeza kwenye shughuli za ujasiriamali.

Khadija Kopa akitoa burudani kwa wageni waalikwa.

Shigongo alishangaa kufurika kwa wajane hao na kusema idadi ya wanaume waliokufa inaonekana ni kubwa sana na kumshukuru Makonda kwa kuandaa mipango mbalimbali ya kuwasaidia wananchi wa mkoa wake jambo ambalo halikuwahi kufanywa na viongozi wa nafasi yake waliopita.

Ruby akiburudishwa wageni waalikwa.

“Mungu akubariki sana ndugu yangu Makonda, acha wakuambie unatafuta sifa, acha wakuambie unatafuta umaarufu na mambo mengine lakini upande wangu nakupongeza sana na Mungu akubariki”.

 

Alisema Shigongo na kusapotiwa na umati wa wajane hao kwa kumpigia mayowe baada ya kusema hivyo.

HABARI/ PICHA: RICHARD BUKOS /GPL  

Comments are closed.