The House of Favourite Newspapers

MAKONDA AMPA FID Q MIL 5 AMPELEKEE MAMA WA GODZILLA

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, leo Jumanne, Februari 19, 2019 amemkabidhi rapa Farid Kubanda ‘Fid Q’ kiasi cha Tsh milioni 5 ili ampelekee Mama mzazi wa aliyekuwa rapa wa Bongo, Marehemu Godzilla.

 

Mama Godzilla alidai kwamba marehemu mwanaye alikuwa ana mpango wa kumfungulia duka la dawa (pharmacy) na tayari alishampatia Tsh milioni 4, lakini pesa hiyo aliitumia tena kwa matibabu ya marehemu.

Baada ya kusikia hilo, RC Makonda alimfuta machozi mama huyo na kumuahidi kumkabidhi Fid Q pesa hiyo ili mama atimize ndoto yake kitu ambacho amekitekeleza leo.

Comments are closed.