The House of Favourite Newspapers

MAKONDA AVAMIA MABONDENI KIBURUGWA, AWATAKA WAHAME MARA MOJA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza jambo.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo amevamia mabondeni Kiburugwa, Kilungule na maeneo mengine kwa ajili ya kuwahimiza Wananchi wote waliojenga kwenye maeneo hatatishi ikiwemo mabonde na sehemu zenye miinuko kuondoka ili kuzuia vifo visivyokuwa na ulazima.

 

Makonda ametoa kauli hiyo leo wakati alipofanya ziara ya kukagua uharibifu wa nyumba zilizovunjika maeneo hayo  baada ya wakazi kujenga kwenye maeneo yasiyoruhusiwa.

Aidha Makonda amewaagiza Wenyeviti wote wa mitaa kuainisha nyumba zilizojengwa kwenye maeneo hatarishi ambapo amewataka kutoruhisu watu kuendelea kujenga maeneo ya mabondeni.

Katika kutafuta mwarobaini wa tatizo la wananchi waishio mabondeni Makonda ameandaa mkutano wa wananchi wote waishio maeneo ya mabondeni kwaajili ya suluhisho la kudumu.

Katika ziara hiyo amejionea nyumba nyingi zikiwa zimejengwa kwenye maeneo yasiyo rasmi kiasi kwamba hata ikitokea janga la moto inakuwa vigumu Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kufika na hata mgonjwa akizidiwa gafla kuwa vigumu kuwahishwa hospital jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao.

Comments are closed.