The House of Favourite Newspapers

Makonda: Nimepokea Meseji Zaidi ya 5000, Majina 100 ya Mashoga

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema ameanza kupata mrejesho ikiwa ni siku moja tu tangu atangaze kampeni ya kuanza kuwakamata mashoga pamoja na malaya ambao wanajiuza kupitia mitandao ya kijamii.
Hatua hiyo imekuja baada ya msanii wa muziki, Amber Rutty kuachia video chafu mtandaoni hali ambayo ilimfanya mkuu huyo kutoa tamko la kutaka akamatwe.
RC Makonda alisema kwa tukio ambalo amelifanya msichana huyo anapaswa kufungwa jela, kwani ni ukiukwaji wa sheria za nchi huku akiwataka Wanadar es salaam kumtumia majina ya mashoga pamoja na watu ambao wanafanya biashara ya ngono mtandaoni.
“Nimepokea msg zaidi 5,763 na majina ya Mashoga zaidi ya 100 hii inaonyesha Wana DSM hawataki laana ya mashonga. Naendelea kupokea majina ya Mashoga,” amesema RC Makonda kupitia taarifa aliyoitoa leo.
Mkuu huyo amesema msako mkali wa kamata kamata ya mashoga na watu wanaojiuza utaanza wiki ijayo kwani kwa sasa anakiandaa kikosi kazi pamoja na kupokea baadhi ya majina.

ITAKULIZA: Familia walipoona jeneza la Isaac Gamba, VILIO!!

Comments are closed.