The House of Favourite Newspapers

MAKUNDI Ligi la Vijana Under 20 (Uhai Cup 2018) Haya Hapa

 

DROO ya upangaji wa makundi kwa timu 16 zitakazoshiriki ligi ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (U20) ijulikanayo kwa jina la ‘Uhai Cup’ imefanyika leo ndani ya studio za Azam TV.

 

Ligi hiyo inayoanza rasmi Juni 9, mwaka huu katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma jijini Dodoma itashirikisha timu za vijana wenye umri huo kutoka katika vilabu vilivyoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliomalizika hivi karibuni.

 

Na haya ndiyo Makundi yenyewe.

Kundi A: Yanga, Ruvu Shooting, Mbeya City, Mbao FC.

Kundi B: Simba, Singida United, Stand United, Njombe Mji.

Kundi C: Azam, Mtibwa Sugar, Mwadui FC, Majimaji FC.

Kundi D: TZ Prisons, Lipuli FC, Kagera Sugar, Ndanda FC.

 

Azam TV ambao ni wadhamini wa ligi hiyo kwa upande wa matangazo ya Televisheni, itakurushia mechi zote mbashara, ambapo kwa mujibu wa ratiba, kutakuwa na mechi mbili kila siku, ya kwanza ikianza saa 8:00 mchana na mechi ya pili ikianza saa 10:00 jioni.

Comments are closed.