The House of Favourite Newspapers

Mama Maria Nyerere na Mama Janeth Magufuli Waadhimisha Miaka 100 ya Baba wa Taifa

0

Mjane wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Maria Nyerere pamoja na Mjane wa Rais wa Awamu ya Tano Mama Janeth Magufuli wamehudhuria ibada maalum katika kanisa la St Peters kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere akiwa na Mama Janeth Magufuli mjane wa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Jenista Mhagama wakishiriki katika Misa Maalumu ya kuadhimisha Miaka 100 ya Kuzaliwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam Jumamosi Aprili 23, 2022
Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere akiwa na Mama Janeth Magufuli Mjane wa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Jenista Mhagama wakitoka nje na kusalimiana na watu baada ya kushiriki katika Misa Maalumu ya kuadhimisha Miaka 100 ya Kuzaliwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam Jumamosi Aprili 23, 2022

 

 

Leave A Reply