The House of Favourite Newspapers

MAMA MOBETTO AAPA KUSIMAMA NYUMA YA MWANAYE

 

Hamisa Mobetto, Shufaa Rutiginga

MAMA wa mwana-mitindo Hamisa Mobetto, Shufaa Rutiginga ameweka wazi kuwa hata kama watu wote watamtenga mwanaye huyo, lakini yeye atasimama nyuma yake siku zote bila kujali watu wanambeza kwani anajua uchungu wake. Mama Mobetto aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, watu wakie-ndelea kumzushia mwanaye mabaya na kumsema kila kukicha kazi yake yeye siku zote ni kumpa moyo na kumsihi asikate tamaa.

“Kazi yangu kubwa kwa mtoto wangu ni kumpa moyo na kumuonesha ni jinsi gani ninampenda maana naamini ni changamoto tu anapitia, lakini zitaisha na zitamfanya kusimama imara,” alisema mama Mobetto.

MEMORISE RICHARD

Comments are closed.