IKIWA ni mwaka wa sita tangu tasnia ya filamu nchini impoteze staa wa filamu, Steven Kanumba, ‘The Great’, wanafamilia, ndugu, jamaa pamoja na marafiki, wameungana na kufanya ibada katika kaburi la leke lililopo Makaburi ya Kinondoni jijini Dar ikiwa ni ishara ya kumkubuka, kumuombea na kuenzi kazi yake.
Ibada hiyo imeongozwa na Msanii wa filamu, Emmanuel Myamba maarufu kama Pastor Myamba ambaye katika mahubiri yake amesema marehemu Kanumba atakumbukwa daima kutokana na enzi za uhai wake kuiinua tasnia ya filamu kutoka kitaifa mpaka kuvuka mipaka ya Tanzania na kuifanya iheshimike na kuthaminiwa miongoni mwa mataifa makubwa duniani.
Kanumba alifariki dunia Aprili 7, 2012 nyumbani kwake maeneo ya Vatcan-Sinza jijini Dar baada ya ugomvi kati yake na aliyekuwa mpenzi wake kwa siri, staa wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka mitatu katika Gereza la Segerea kwakuhusika na kifo hicho.
Comments are closed.